Tarafa ya Moipo yaadhimisha Mei Mosi Kibabe
Tarafa Moipo iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Simanjiro imeadhimisha sikukuu ya wafanyakazi duniani maarufu kama Mei Mosi kwa shughuli mbalimbali za burudani.
Awali,akifungua sherehe hizo,Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Ndugu, Gracian Makota, ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi, amewaasa watumishi kuwa wavumilivu katika kufikia malengo yao na kujiepusha na tamaa za mafanikio ya haraka.Adha ndugu Makota amewasihi watumishi kuendeleza mshikamano na umoja miongoni mwao ili kuongeza tija sehemu za kazi.
Sherehe hizo zilizoandaliwa na vyama vya wafanyakazi kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za serikali pamoja na sekta binafsi zilipambwa kwa michezo ya aina mbalimbali kwa kushirikiana na watumishi na wananchi wa Mirerani katika viwanja vya Mnyalu Complex Mirerani.Wafanyakazi walishindana katika mchezo wa kukuna nazi,kuvuta kamba, kula,kufukuza kuku,netboli pamoja na mpira wa wavu.
Baadhi ya taasisi zilizoshiriki maadhimisho hayo ni pamoja na benki za NMB na CRDB, pia taasisi ya TAKUKURU,WIZARA YA MADINI,SHULE BINAFSI pamoja na vyama vya wafanyakazi CWT,CHAKUHAWATA na TALGWU.
Maadhimisho ya Mei Mosi husheherekewa kila mwaka kote duniani,ikikutanisha wafanyanyakazi wa sekta binafsi na umma kuonesha mshikamano na umoja miongoni mwao na kutafakari kuhusu utumishi wao.



No comments:
Post a Comment